21. Dalili juu ya ulazima kupangilia na Muwaalaah

Mtunzi amesema:

“Dalili ya kupangilia.”

Ni kwamba Allaah (Ta´ala) katika Aayah inayozungumzia wudhuu´ ameingiza viungo vinavyooshwa baina ya maosho, kama tulivyotangulia kusema.

Mtunzi amesema:

Dalili ya kupangilia ni Hadiyth:

 “Anza kwa Alichoanza nacho Allaah.”[1]

imetupa faida juu ya ulazima wa kutawadha kwa kupangilia, kama alivotaja Allaah.

Maneno yake mtunzi:

“Na dalili ya Muwaalaah ni Hadiyth ya mtu aliyeacha sehemu bila ya kuosha. Imepokelewa kwamba wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona mtu aliyeacha sehemu katika mguu wake kiasi cha dirhamu hakikufikiwa na maji, hivyo akamuamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kurudia na kutia wudhuu´ upya. Khaalid amepokea kutoka kwa baadhi ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtume alimwona bwana mmoja akiswali na nyuma ya mgongo wake kuna kiasi cha dirhamu hakikufikiwa na maji. Basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha arudi kutawadha na kuswali.”

Endapo Muwaalaah ingekuwa sio lazima basi ingelitosha kuosha sehemu ile peke yake.

[1] an-Nasaa’iy (2962). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Tamaam-ul-Minnah”, uk. 88.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 15/12/2021