20. Dalili juu ya kwamba faradhi za wudhuu´ ni sita

Mtunzi amesema:

Dalili ya hilo ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَينِ

“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni.”[1]

Dalili ya hilo – Hizi ni dalili juu ya kwamba faradhi za wudhuu´ ni sita. Maneno Yake:

إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ

“Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni… “

yamekusanya zile hali zote anazosimama msimamaji ndani ya swalah ingawa ni amri ambayo amelazimishwa kuosha yale ambayo Allaah ameamrisha kuyaosha kwa yule mwenye kusimama kwa ajili ya swalah baada ya kupata hadathi yenye kumchengulia twahara yake[2].

Katika Aayah ipo dalili ya kuoshwa kwa viungo vinne na kwamba vinatakiwa kupangiliwa.

[1] 05:06

[2] Tafsiyr-ut-Twabariy (06/114).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 31
  • Imechapishwa: 15/12/2021