372 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Wanaume wawili kutoka Bulayy, wilaya ya Qudhwaa´ah, walisilimu pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mmoja wao akafa hali ya kuwa ni shahidi na mwingine akaishi zaidi kwa mwaka mmoja. Twalhah bin ´Ubaydillaah akasema: “Nikaota kuhusu Pepo na nikamuona yule mwingine anaingizwa Peponi kabla ya yule aliyekufa shahidi, jambo ambalo lilinistaajabisha. Nikamweleza hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – au Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitajiwa jambo hilo – ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

أليسَ قد صام بعدَه رمضانَ، وصلى سِتةَ آلافِ ركعةٍ، وكذا وكذا ركعةً، [صلاةَ] سَنةٍ

“Je, si alifunga Ramadhaan na akaswali Rak´ah elfu sita mwaka mzima baada yake?”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri.

373 – Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” yake na al-Bayhaqiy wmaepokea mfano wake, ikiwa refu zaidi, kupitia kwa Twalhah. Ibn Maajah na Ibn Hibbaan wamezidisha mwishoni mwake:

فَلَمَا بينهما أبعدُ مما بين السماءِ والأرضِ

“Umbali uliopo baina yao ni mkubwa zaidi kuliko umbali wa mbingu na ardhi.”[2]

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/273)
  • Imechapishwa: 30/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy