Swali: Imesihi kwamba Rabiy´ah al-´Adawiy amesema kuwa anamwabudu Allaah kwa sababu ya kumpenda na hataraji Pepo Yake wala haogopi Moto Wake?

Jibu: Haya yanasimuliwa kutoka kwake. Haya, kama yamesihi kutoka kwake, ni kutokana na ujinga wake. Ni kutokana na ujinga wake. Mitume na Manabii (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wamemwabudu Allaah hali ya kuogopa adhabu Yake na kutaraji rehema Zake. Lakini, kama yamesihi amesema hivo, yanajulisha juu ya ujinga wake na kwamba alikuwa mfanya ´ibaadah mjinga. Allaah amesema kuhusu Mitume, Manabii na waja wema:

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.”[1]

Amesema vilevile:

وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ

“Kwa wale mwenye kukhofu kusimama mbele ya Mola wake atapata bustani mbili.”[2]

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”[3]

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا

 “Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza, na wanataraji rehema Zake na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ni ya kutahadhariwa daima.”[4]  

Namna hii ndivo wanavokuwa mawalii wa Allaah katika Mitume na waja wema. Wanamwabudu, wanamtakasia nia hali ya kumpenda, kumtaraji na kumukhofu vyote kwa pamoja. Asiyemuogopa Allaah hakuna kheri wala dini kwake.

[1] 21:90

[2] 55:46

[3] 18:110

[4] 17:57

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22860/حكم-ما-نسب-رابعة-اعبد-الله-محبة-لا-للجنة
  • Imechapishwa: 30/08/2023