Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya jua na mwezi ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

“Na katika ishara Zake ni usiku na mchana na jua na mwezi. Hivyo basi, msisujudie jua na wala mwezi, bali msujudieni Allaah ambaye aliyeviumba [hivyo] ikiwa Yeye pekee mnawambudu.”[1]

MAELEZO

Dalili ya kuabudu kwao jua na mwezi ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

”Na katika alama Zake ni usiku na mchana, jua na mwezi. Hivyo basi msisujudie jua na wala mwezi, bali msujudieni Allaah ambaye aliyeviumba – ikiwa Yeye Pekee ndiye mnamwabudu.”[2]

Akawakataza kumwabudu kwao asiyekuwa Muumba:

لَا تَسْجُدُوا

“… msisujudie… “

Sambamba na hilo akawaamrisha wamwabudu Yeye pekee kwa kusema:

وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ

”… msujudieni Allaah ambaye aliyeviumba .”

[1] 41:37

[2] 41:37

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 142
  • Imechapishwa: 12/03/2023