Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya Malaika ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا

“Na wala hakuamuruni kuwafanya Malaika na Manabii kuwafanya miungu.”[1]

MAELEZO

Dalili ya makatazo ya kuwaabudu Malaika ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا

“Na wala hakuamuruni kuwafanya Malaika na Manabii kuwafanya miungu.”[2]

Amesema (Ta´ala):

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَـٰؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ قَالُوا سُبْحَانَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِم ۖ بَلْ كَانُوا يَعْبُدُونَ الْجِنَّ ۖ أَكْثَرُهُم بِهِم مُّؤْمِنُونَ

“Siku atakayowakusanya wote kisha atawaambia Malaika: “Je, hawa  ndio waliokuwa wakikuabuduni?” Watasema: “Utakasifu ni Wako!” Wewe ni mlinzi badala yao! Bali walikuwa wakiabudu majini, wengi wao wakiwaamini.”[3]

[1] 03:80

[2] 03:80

[3] 34:40-41

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 143
  • Imechapishwa: 12/03/2023