19. Mtume aliwapiga vita waliokuwa wakiabudu waungu mbalimbali

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Msingi wa tatu ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja kwa watu waliokuwa ni wenye kutofautiana katika ´ibaadah zao. Miongoni mwao kuna ambao walikuwa wakiabudu Malaika, wengine walikuwa wakiwaabudu Mitume na waja wema, wengine wakiabudu mawe na miti na wengine wakiabudu mwezi na jua. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita na hakutofautisha kati yao. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.”[1]

MAELEZO

Allaah alimtuma Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ambao wametofautiana katika ´ibaadah zao. Miongoni mwao wako waliokuwa wakiabudu masanamu, miti, mawe na jua, mwezi. Wengine wakiwaabudu Mitume, mawalii na waja wema. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawakufurisha na akahalalisha kuuliwa na kuchukua mali yao. Aliwapiga vita wote. Amesema (Ta´ala):

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko shirki na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.”[2]

Fitina ni shirki. Kwa maana nyingine Aayah inasema kuwa awapige vita mpaka shirki itokomee. Hakutofautisha kati yao.

Kwa hivyo mwenye kuabudu miti, mawe, jua, mwezi, waja wema au Malaika wote ni washirikina na wote wanatakiwa kupigwa vita. Wote wako katika batili. Kila mwenye kumwabudu asiyekuwa Allaah ni mshirikina na kafiri. Mtunzi wa kitabu ameleta dalili ya aina zote hizi.

[1] 08:39

[2] 08:39

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 141
  • Imechapishwa: 12/03/2023