Ni ipi Haniyfiyyah ambayo ni dini ya Ibraahiym? Jibu mtunzi amefasiri kuwa Haniyfiyyah ya kwamba ni kumwabudu Allaah na kumtekelezea ´ibaadah Allaah. Unatakiwa umwabudu Allaah kwa swalah, swawm, hajj, du´aa, kuchinjwa, nadhiri, kuwatendea wema wazazi, kuwaunga ndugu, kuwatendea wema majirani, kupambana jihaad katika njia ya Allaah, kuamrisha mema na kukataza maovu, kuizuia nafsi kutokamana na machafu na mambo mengine ya haramu. Kwa hivyo unatakiwa kumwabudu Allaah hli ya kumtakasia Yeye dini. ´Ibaadah peke yake haitoshi. Bali ni lazima iambatane na kumtakasia nia Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 36
  • Imechapishwa: 05/02/2023