194 – Ibn ´Abbaas amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

وعن ابن عباس قال: قال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ”  أتاني الليلةَ رَبِّي [في أحسن صورة، فـ] قال: يا محمد! أتدري فِيمَ يختصم الملأُ الأعلى؟ قلتُ: نعم؛ في الكفّارات والدّرجاتِ، ونَقْلِ الأقدام للجماعاتِ، وإسباغِ الوضوء في السَّبَرات ، وانتظارِ الصلاةِ بعد الصلاةِ، ومن حافظ عليهِنَّ عاشَ بخيرٍ، وماتَ بخيرٍ، وكان من ذنوبه كيومَ ولدته أمه.

“Leo usiku Mola wangu amenijia katika umbo zuri kabisa[1] na akasema: “Ee Muhammad! Unajua ni nini wanachobishana juu ya ulimwengu wa juu?” Nikasema: “Ndio. Juu ya kafara na ngazi, nyayo kwenda katika swalah za mikusanyiko, kueneza vizuri wudhuu´ wakati wa baridi kali, kusubiri swalah baada kumaliza swalah nyingine na mwenye kuzihifadhi basi huisi na kufa vizuri ambapo anakuwa msafi kutokana na madhambi kama ile siku aliyozaliwa na mama yake.”[2]

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyh ni nzuri.”

[1] Ujio huu ilikuwa usingizini.

[2] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/196-197)
  • Imechapishwa: 27/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy