Njia za ulinganizi kwa mtazamo wa Ibn Baaz

Swali: Njia za ulinganizi ni kwa mujibu wa Qur-aan au Sunnah (توقيفية) au ni kwa ijtihaad tu ya mtu?

Jibu: Njia za ulinganizi ni kwa ijtihaad tu ya mtu na sio kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Ambacho ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni kuwa na elimu:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata.” (12:108)

Akiwa na elimu basi anaweza kulingania kwa Allaah kwa kuandika, kuongea, kwa simu au kwa njia nyingine yoyote anayoiweza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23329/هل-وساىل-الدعوة-توقيفية-ام-اجتهادية
  • Imechapishwa: 27/12/2023