19. Hadiyth ”Awe mbali ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie… “

19 – Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia: Ibn Abiy Maryam ametuhadithia: Muhammad bin Hilâl ametuhadithia: Sa´d bin Ishaaq bin Ka´b bin ´Ujrah amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ka´b bin ´Ujrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

احضروا المنبر، فحضرنا، فلما ارتقى الدرجة قال: آمين، ثم ارتقى الدرجة الثانية فقال: آمين، ثم ارتقى الدرجة الثالثة فقال: آمين، فلما فرغ نزل عن المنبر، قال: فقلنا له: يا رسول الله لقد سمعنا منك اليوم شيئاً ما كنا نسمعه قال: إن جبريل عرض لي فقال: بعد من أدرك رمضان فلم يغفر له، فقلت: آمين، فلما رقيت الثانية قال: بعد من ذكرت عنده فلم يصلِّ عليك، فقلت: آمين، فلما رقيت الثالثة قال: بعد من أدرك أبويه الكبر أو أحدهما فلم يدخلاه الجنة، فقلت آمين

”Nileteeni mimbari.” Tukamletea. Alipopanda ngazi ya kwanza akasema: ”Aamiyn.” Kisha akapanda ngazi ya pili na kusema: ”Aamiyn.” Halafu akapanda ngazi ya tatu na kusema: ”Aamiyn.” Alipomaliza akashuka kutoka juu ya mimbari ambapo tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah, hii leo tumesikia kitu ambacho tulikuwa hatukisikii hapo kabla.” Akasema: ”Jibriyl amejionyesha kwangu akasema: ”Awe mbali ambaye atakutana na Ramadhaan na asisamehewe.” Nikasema: ”Aamiyn.” Nilipopanda ya pili akasema: ”Awe mbali ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.”  Nilipopanda ya tatu akasema: ”Awe mbali ambaye atakutana na wazazi wake katika hali ya utuuzima wao, au mmoja wao, kisha wasimwingize Peponi.” Nikasema: ”Aamiyn.”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh kupitia zilizotangulia zinazoitia nguvu. Ameipokea al-Haakim na akaisahihisha. Inayo nyingin inayoitia nguvu kwa Ibn Hibbaan (2382).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 06/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy