18. Hadiyth ”Liguse mchanga pua la mja ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie… “

18 – Abu Thaabit ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Haazim ametuhadithia, kutoka kwa Kathiyr bin Zayd, kutoka kwa al-Waliyd bin Rabaah, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesimulia:

أن رسول الله صلى الله عليه وسلم رقي المنبر فقال: آمين، آمين، أمين، فقيل له: يا رسول الله ما كنت تصنع هذا فقال: قال لي جبريل: رغم أنف عبد دخل عليه رمضان لم يغفر له، فقلت: آمين، ثم قال: رغم أنف عبد أدرك أبويه أو أحدهما لم يدخلاه الجنة، فقلت آمين، ثم قال: رغم أنف عبد ذكرت عنده فلم يصل عليك، فقلت، آمين.

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda kwenye mimbari akasema: ”Aamiyn. Aamiyn. Aamiyn.” Swahabah mmoja akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, hukuwa mwenye kufanya hivo?” Akasema: ”Jibriyl amenambia: ”Liguse mchanga pua la mja ambaye atafikiwa na Ramadhaan na asisamehewe.” Nikasema: ”Aamiyn.” Kisha akasema: ”Liguse mchanga pua la mja ambaye atakutana na wazazi wake, au mmoja wao, na wasimwingize Peponi.” Nikasema: ”Aamiyn.” Halafu akasema: ”Liguse mchanga pua la mja ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri. Abu Thaabit jina lake ni Muhammad bin ´Ubaydillaah bin Muhammad al-Madaniy. Hadiyth ameipokea Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” zao.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 34
  • Imechapishwa: 06/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy