01. Hadiyth “Lau kama sio kuwatia uzito ummah wangu… “

205 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لولا أنْ أَشُقَّ على أُمتي لأمرتُهم بالسِّواك مع كلِّ صلاةٍ

“Lau kama sio kuwatia uzito ummah wangu, basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila wudhuu´.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, ambaye tamko ni lake, na kwa Muslim imekuja:

لولا أنْ أَشُقَّ على أُمتي لأمرتُهم بالسِّواك عند كل صلاة

“Lau kama sio kuwatia uzito ummah wangu, basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”

Kwa an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” imekuja:

لولا أنْ أَشُقَّ على أُمتي لأمرتُهم بالسِّواك مع الوضوء عند كل صلاة

“Lau kama sio kuwatia uzito ummah wangu, basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak na kutawadha wakati wa kila swalah.”[2]

 Ahmad na Ibn Khuzaymah wameipokea katika ”as-Swahiyh” yake:

لولا أنْ أَشُقَّ على أُمتي لأمرتُهم بالسِّواك مع كلِّ وضُوءٍ

“Lau kama sio kuwatia uzito ummah wangu, basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila wudhuu´.”[3]

[1] Swahiyh.

[2] Nzuri na Swahiyh.

[3] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/202)
  • Imechapishwa: 05/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy