20. Hadiyth ”Bwana mmoja kila asubuhi alikuwa akitembelea kaburi la Mtume na akimswalia…. “

20 – Ja´far bin Ibraahiym bin Muhammad bin ´Aliy bin ´Abdillaah bin Ja´far bin Abiy Twaalib ametuhadithia, kutoka kwa bwana mmoja wa mji aliye aliyemukhabarisha, kutoka kwa ´Aliy bin Husayn bin ´Aliy, ambaye amesema: ”Bwana mmoja kila asubuhi alikuwa akitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akimswalia, ´Aliy bin Husayn akamuona. ´Aliy bin Husayn akamwambia: ”Ni kipi kinachokupelekea wewe kufanya hivo?” Akasema: ”Mimi napenda kumtakia amani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Aliy bin al-Husayn akamwambia: ”Je, nisikueleze jambo kutoka kwa baba yangu?” Akasema: ”Ndio.”  ´Aliy bin al-Husayn akamwambia: ”Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa babu yangu, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لا تجعلوا قبري عيداً، ولا تجعلوا بيوتكم قبوراً، وصلوا علي وسلموا حيثما كنتم، فسيبلغني سلامكم وصلاتكم

”Msilifanye kaburi langu kuwa ni lenye kutembelewa mara kwa mara na msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi. Niswalieni na mnitakie amani popote mnapokuwa. Hufikishiwa amani na swalah zenu.”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh kwa njia zake na nyenginezo zenye kuitia nguvu, baadhi yazo zitakuja katika (30). Nimezihakiki katika “Tahdhiyr-us-Saajid”, uk. 98-99.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 06/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy