18. Hadiyth “Kueneza vizuri wudhuu´ wakati wa shida… “

193 – Ameipokea Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ألا أدلّكم على ما يُكَفِّرُ اللهُ به الخطايا، ويزيد به في الحسناتِ، وُيكَفِّر به الذنوبَ؟

قالوا: بلى يا رسول الله! قال: “إسباغُ الوضوءِ على المكروهاتِ، وكثرةُ الخُطا إلى المساجدِ، وانتظارُ

“. الصلاةِ بعد الصلاةِ، فذلكُم الرباط

“Je, nisikujuzeni kitu ambacho Allaah kwacho anafuta makosa, kuongeza kwacho mema na kufuta kwacho madhambi?” Wakasema: “Bila shaka, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Kueneza vizuri wudhuu´ wakati wa shida, hatua nyingi kwenda misikitini na kusubiri swalah baada ya kumaliza swalah nyingine. Huko ndio kulinda mipaka ya nchi.”[1]

Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Shurahbiyl bin Sa´d, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/261)
  • Imechapishwa: 26/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy