Ni lazima kuvua viatu wakati wa kuingia makaburini?

Swali: Je, ni jambo la lazima kuvua viatu wakati wa kuingia makaburini?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kuvivua. Isipokuwa ikiwa kuna haja; jua kali, miba n.k. Kwa msemo mwingine haja imepelekea kupita. Vinginevyo mtu anapaswa kuvivua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Ee mwenye viatu. Vua viatu vyako!”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23322/هل-يجب-خلع-النعال-اثناء-دخول-المقابر
  • Imechapishwa: 26/12/2023