17. Swahabah wa kike aliyeonyesha uso na mikono yake

07 – Subay´ah bint al-Haarith ameeleza:

”Aliolewa na Sa´d bin Khawlah (ambaye alikufa katika vita vya Badr) katika vita vya Kuaga. Kabla ya kumalizika eda yake ya miezi minne na siku kumi akajifungua mtoto. Baada ya damu yake ya uzazi akakutana na Abus-Sanaabil bin Ba´kak. Alikuwa ameweka wanja machoni, amejipaka rangi na kujiandaa. Akamwambia maneno kama: ”Tulia. Pengine unataka kuolewa? Eda ilikuwa miezi minne na siku kumi tangu afariki mume wako.” Akasema: ”Nikamwendea Mtume (Swalla Alllaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza aliyoyasema Abus-Sanaabil bin Ba´kak. Akasema: ”Ilimalizika wakati ulipojifungua.”[1]

[1] Ahmad (6/432) kupitia njia mbili, moja ni Swahiyh na nyingine ni nzuri. Asili ya Hadiyth hiyo imepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim na wengineo:

”Alikuwa amejipamba kwa ajili ya posa.

Ndani yake imetajwa kuwa Abus-Sanaabil alikuwa amemchumbia lakini akakataa. Kwa an-Nasaa´iy imekuja:

”Alikuwa akitarajia kuolewa tena.”

Hadiyth ni dalili ya wazi juu ya kwamba mikono ya wanawake haikuwa uchi kwa mujibu wa desturi ya Maswahabah wa kike. Vivyo hivyo uso na angalau kwa uchache macho. Vinginevyo Subay´ah (Radhiya Allaahu ´anhaa) asingejidhihirisha namna hiyo mbele ya Abus-Sanaabil, na khaswakhaswa alikuwa amemposa lakini akakataa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 69
  • Imechapishwa: 10/09/2023