17. Kumg´oa maiti meno yake ya dhahabu au ya fedha

Swali 17: Meno ya maiti yang´olewe akifa ilihali yuko na meno ya dhahabu kama yuko na deni ijapo kung´olewa kwake si kwa urahisi au yaachwe akiwa yuko na deni?

Jibu: Maiti akifa na yuko na meno ya dhahabu au fedha na kung´olewa kwake si kwa urahisi, basi hapana neno kuyaacha. Ni mamoja ni mwenye deni au hana deni. Kama kuna uwezekano yang´olewe baada ya muda na wapewe warithi au kulipwe deni. Lakini ikiwa kuna wepesi wa kufanya hivo basi italazimika. Kwa sababu ni mali ambayo haitakiwi kuipoteza kukiwa kuna uwezo wa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 20
  • Imechapishwa: 14/12/2021