296 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallaam) amesema:

سيكون في آخر الزمان قومٌ يكون حديثهم في مساجدهم، ليس لله فيهم حاجة

“Katika zama za mwisho watakuwepo watu ambao mazungumzo yao watafanya kwenye misikiti yao. Allaah hana haja na watu hao.”[1]

Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/238)
  • Imechapishwa: 16/11/2022