17. Dalili ya kwamba haifai kwa muumini kumpenda kafiri

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao. Hao [Allaah] amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake na atawaingiza kwenye mabustani yapitayo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.”[1]

MAELEZO

Aayah hizi kutoka katika Suurah “al-Mujaadalah” ni dalili juu ya yale yaliyotangulia. Hutompata muumini anajenga urafiki na kafiri na kumpenda. Akijenga urafiki na kumpenda kafiri basi anakuwa kama yeye. Akimpenda kafiri kwa sababu ya ukafiri wake basi anakuwa kafiri kama yeye:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara kuwa ni marafiki – wao kwa wao ni marafiki. Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao, basi hakika yeye ni miongoni mwao.”[2]

Atakayewapenda kwa sababu ya dini yao basi naye ni mmoja wao.

Waumini hawawapendi makafiri hata kama ni katika baba zao, mtoto wake, ndugu yake au atakuwa katika jamaa zake. Waumini hawawapendi isipokuwa waumini wenzao. Waumini wanapenda kwa ajili ya Allaah na wanachukia kwa ajili ya Allaah. Hivyo ndivo imani inathibiti kwenye mioyo yao. Allaah huwatia nguvu kwa roho kutoka Kwake kwa sababu wamenyooka katika kumtii Allaah, wakapenda kwa ajili ya Allaah, wakachukia kwa ajili ya Allaah. Matokeo yake Allaah (Subhaanah) akawatia nguvu kwa Malaika Wake na kutokana na ile imani aliyoiweka kwenye nyoyo zao.

Maneno Yake (Ta´ala):

وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“… na atawaingiza kwenye mabustani yapitayo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.”

Hizi ndio thawabu na malipo yao. Maana yake ni kwamba hawatotoka na wala kuiacha Pepo.

Katika Aayah kuna kuthibitisha kuridhia kwa Allaah. Allaah amewaridhia kwa sababu wamempwekesha na kumtakasia Yeye ´ibaadah. Allaah amewahalalishia Pepo. Kundi la Allaah ndio mawalii na wapenzi Wake. Kundi la shaytwaan ni wale ambao wanawapenda makafiri na kujenga urafiki nao. Hawa wamekhasirika kutokana na yale mapenzi waliyowapa makafiri. Hivyo wakafanana nao na wakakanushiwa imani.

[1] 58:22

[2] 05:51

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 04/02/2023