Makafiri wamegawanyika sampuli mbili:

1 – Wapiganaji vita. Bi maana wale wanaotupiga vita. Hawa tunatakiwa kuwapiga vita. Hakuna kati yetu sisi na wao isipokuwa vita. Hapewi chakula wala kinywaji. Bali anatakiwa kuachwa mmoja wao pale anaposhikwa na njaa kwa sababu ni adui yako na anakupiga vita.

2 – Wasiokuwa wapiganaji. Nao ni wale waliopewa amaani. Kati yetu sisi na wao kuna mkataba wa amani. Kwa mfano aingie ndani ya nchi kwa mkataba wa usalama au wa amani. Wanatakiwa kupewa amani. Makafiri aina hii hawapigwi vita na wala hawatoki nje ya nchi yetu. Vilevile hapana vibaya kuwatendea wema na kuwavisha. Hata hivyo haitakiwi kwetu kuwapenda mapenzi ya kidini. Bali tuwachukie na kuamini kuwa ni makafiri na kwamba ni maadui wa Allaah. Aidha tunatakiwa kujitenga mbali na dini yao. Lakini tunawatendea wema, tunawapa chakula na kinywaji na mema mengine. Pengine katika kufanya hivo ikawa ni miongoni mwa sababu za wao kuingia katika Uislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema ndani ya Kitabu Chake kitukufu:

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

”Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu – hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu. Hakika si vyengine Allaah anakukatazeni juu ya wale waliokupigeni vita katika dini na wakakutoeni kutoka majumbani mwenu na wakasaidiana juu ya kukutoeni [ndio anaokukatazeni] kufanya urafiki nao. Na yeyote atakayewafanya marafiki basi hao ndio madhalimu!”[1]

[1] 60:08-09

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 32
  • Imechapishwa: 04/02/2023