Swali: Je, inafaa kuswali Rak´ah nne baada ya ´Aswr kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliziswali baadhi ya nyakati? Inafaa kwa mwingine kuziswali?

Jibu: Hapana, hizi ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Allaah amrehemu mwenye kuswali [Rak´ah] nne kabla ya ´Aswr.”

Kuhusu baada yake haifai. Hizo ni miongoni mwa mambo maalum yanayomuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22314/حكم-التنفل-بعد-صلاة-العصر
  • Imechapishwa: 04/02/2023