2 – Uombezi wenye kuthibitishwa. Ni ule ambao unaombwa kutoka kwa Allaah. Uombezi huu ni wa haki.

Mfano wa uombezi wenye kuthibitishwa ni pale ambapo mja anamuomba Allaah amfanye Mtume Wake kumuombea na wakati huohuo mwombewaji akawa ni miongoni mwa wapwekeshaji. Uhakika wake ni kwamba mwombeaji amekirimiwa uombezi. Kwa hivyo Allaah anamkirimu mwombeaji kwa kumpa idhini. Vinginevyo fadhilah inarudi kwa Allaah (Subhaanah).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 139
  • Imechapishwa: 06/03/2023