16. Dalili ya aina ya kwanza ya uombezi wenye kukanushwa

Dalili ya uombezi wenye kukanushwa:

1 – Maneno Yake (Ta´ala):

مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“… kabla haijafika Siku ambayo hakutakuweko mapatano [ya fidya] humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri wao ndio madhalimu.”[1]

2 – Maneno Yake (Ta´ala):

مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ

“Madhalimu hawatokuwa na rafiki na wala mwombezi anayetiiwa.”[2]

3 – Maneno Yake (Ta´ala):

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi.”[3]

4 – Maneno Yake (Ta´ala):

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ

“Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile na wala haitakubaliwa kutoka kwake uombezi na wala hakitachukuliwa kutoka kwake kikomboleo na wala hawatanusuriwa.”[4]

Yule mwenye kufa juu ya ukafiri hatofanyiwa uombezi. Hakika si vyenginevyo watakaoombewa ni wale waliokuwa wakimwabudu Allaah pekee.

[1] 02:254

[2] 40:18

[3] 74:48

[4] 02:48

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 139
  • Imechapishwa: 06/03/2023