16. Njia ya Salaf iko wazi kuliko jua mchana kweupee

Kila kundi na madai batili hupata wafuasi na wasaidizi pasi na nyoyo wala uongofu. Kuhusu njia ya Salaf iko wazi kabisa kuliko jua mchana kweupee kutokana na zile dalili zenye kukata na hoja zenye kung´aa imesimama juu yake kwa kila ambaye ana utambuzi japo kidogo na shauku katika kuitafuta haki.

Allaah amebainisha katika Kitabu kitukufu na Sunnah za Mtume Wake mwaninifu ya kwamba kheri na kufaulu vinapatikana kwa kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah na yale waliyokuwemo Salaf wa Ummah ambao ni Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na wale waliowafuuata kwa wema.

Kwa hiyo walinganizi wa haki wanapaswa kuwaraddi wapotofu hawa kutokana na yale waliyoyajua kutoka katika Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aidha kutokana na yale waliyojifunza kupitia akili zao timamu, utambuzi wao wenye kutekelezeka na maumbile yao yaliyosalimika juu ya uongofu kwa mujibu wa yale waliyojifunza kutoka katika Qur-aan na Sunnah, viumbe vya Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na dalili juu ya uwezo wa Allaah, utukufu Wake, kustahiki Kwake kuabudiwa na ukweli wa Mitume Yake (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na kwamba yale waliyokuja nayo ndio ya haki na ndio yaliyojulishwa na Qur-aan na Sunnah katika kubainisha ya halali na ya haramu, uongofu na upotofu na yale Allaah aliyowawekea katika Shari´ah waja Wake, yale aliyokataza, yale waliyoeleza kuhusu Pepo na Moto na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 16/05/2022