Watu hawa wamepotea upotofu wa mbali kama ambavo wafuasi wa Fir´awn walivopotoshwa na Fir´awn na wafuasi wa Namruud wakapotoshwa na Namruud.

Masikini huyu ambaye anakwenda haja kubwa, anakwenda haja ndogo, anakula, anakunywa na anaumia kwa kila kitu – vipi anaweza kuwa mola? Vipi anakuwa mungu? Vipi haya yatafaa kwake na kwa wafuasi wake? Lakini mambo ni kama alivosema Allaah (Subhaanah):

فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ

“Hakika hayapofuki macho, bali zinazopofuka ni nyoyo ziliomo vifuani.”[1]

أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ

“Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Si vyenginevyo isipokuwa ni kama wanyama.”[2]

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ

”Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake pasi na uongofu kutoka kwa Allaah?”[3]

Vivyo hivyo ad-Dajjaal ambaye atakuja katika zama za mwisho atafuatwa na kundi kubwa katika kila mjinga na kipofu kutokana na ile batili atakayokuwa akisambaza. Atakuja na mambo yasiyokuwa ya kawaida ambayo yatawababaisha wale wanaofanana na wanyama.

[1] 22:46

[2] 25:44

[3] 28:50

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 16/05/2022