Vilevile Bahaaiyyah, Baabiyyah na watu mfano wao ambao wamedai madai batili na wakapotea katika njia hii na wakajivisha mavazi nusu ya wanyama kutokana na yale wanayoita katika batili. Mkuu wao amedai kuwa ni Nabii. Kisha baadaye akadai kuwa yeye ni mola wa walimwengu.

Licha ya kwmaba upotofu wake uko wazi lakini tunaona kuwa yuko na wafuasi, walinganizi na vilabu vinavyosambaza batili yao na kulingania kwayo. Pengine wengi wao wanatambua haki na wanajua kuwa ni mwongo katika madai yake. Lakini hata hivyo anajifanya kuunga mkono batili kutokana na yale malengo alionayo katika maisha haya ya ulimwenguni. Matokeo yake wakawafuata katika njia ya batili. Wamefanan na wanyama. Bali wao wamepotea zaidi kuliko wanyama. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا

“Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Si vyenginevyo isipokuwa ni kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia.”[1]

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ

“Hakika Tumeumba Moto wa Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na watu – wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo na wana macho, lakini hawaoni kwayo na wana masikio, lakini hawasikii kwayo – hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.”[2]

[1] 25:44

[2] 07:179

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 16/05/2022