al-Ikhwaan al-Muslimuun wanatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Baadhi yao utawaona ni wafuasi mashabiki wa madhehebu. Wengine ni Suufiyyah. Wengine ´Aqiydah yao ni Salafiyyah. Vivyo hivyo Jamaa´at-ut-Tabliygh. Hili ni jambo ninalolijua mwenyewe kwa makundi yote mawili.

Wale ambao ni wapwekeshaji na wana ´Aqiydah ya Salafiyyah hawakupata ´Aqiydah hii kutoka katika kundi ambalo wanajinasibisha nalo. al-Ikhwaan al-Muslimuun hawana ´Aqiydah moja ambayo wanaiwajibisha kwa wafuasi wao wote. Kadhalika Jamaa´at-ut-Tabliygh. Hawana chochote katika hayo kabisa. Kwa ajili hiyo utaona namna ambavo makundi yote mawili wamechanganya ´Aqiydah mbalimbali.

Kati ya al-Ikhwaan al-Muslimuun utawakuta ambao ni Ahnaaf, Shaafi´iyyah, Maalikiyyah, Hanaabilah, Ashaa´irah, Maaturiydiyyah na Suufiyyah. Kipindi ambapo al-Ikhwaan al-Muslimuun walikuwa wenye nguvu Misri nilipata kwamba katika ofisi yao ya kibinafsi katika idara walikuwa na baadhi ya Shiy´ah. Wanamkusanya kila muislamu pasi na kutofautisha kati ya Uislamu sahihi na Uislamu uliopotoshwa.

Vivyo hivyo Jamaa´at-ut-Tabliygh. Wao wanachotilia mkazo peke yake ni kuwawaidhi watu na kuwafunza tabia njema, kutodanganya na kuswali misikitini. Hapana shaka kwamba haya ni matendo mazuri, hakuna yeyote anayekwenda kinyume nao, lakini utayapata kwao yale yanayopatikana kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun; Ahnaaf, Shaafi´iyyah, Maalikiyyah, Hanaabilah, Ashaa´irah, Maaturiydiyyah na Suufiyyah, ambao ni wakati na kati na ambao wamechupa mipaka ambao kwa mfano wanaamini Wahdat-ul-Wujuud. Kwa nini? Kwa sababu makundi haya mawili hayana mfumo wa kielimu ambao wanawalingania watu kwao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (2) Dakika: 47.44
  • Imechapishwa: 16/05/2022