Utokaji wa Jamaa´at-ut-Tabliygh hauna msingi katika Sunnah

Muulizaji: Hebu waache wanazuoni watoke pamoja nao – Jamaa´at-ut-Tabliygh – ili wawafunze.

Jibu: Utokaji huu ambao mmezua hauna msingi katika Sunnah. Kuhusu wanazuoni wao wanatoka. Vinginevyo ni kipi kilichotufanya sisi kukujieni? Wakati nilipokuwa naishi Dameski, nilikuwa nikitoka na gari yangu ya zamani – ima mimi mwenyewe na wakati mwingine natoka na baadhi ya ndugu zangu, kama mnavoona wenyewe – kwenda Humus, Hamaa, Halab… yote haya kwa ajili ya Allaah. Sisi tunachotaka ni wanazuoni, wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (540)
  • Imechapishwa: 16/05/2022