Swali 46: Umetaja kwamba mwandamo wa mwezi mpevu wa Ramadhaan na Shawwaal unachelewa nchini Pakistan kwa siku mbili baada ya Saudi Arabia. Je, tufunge pamoja na Saudi Arabia au Pakistan[1]?

Jibu: Kinachonidhihirikia kutoka katika hukumu ya ki-Shari´ah safi ni kwamba ni lazima kwenu kufunga pamoja na waislamu walioko huko kwenu kutokana na mambo mawili yafuatayo:

1 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fungeni siku wengine wanafunga, fungueni siku wengine wanafunga na chinjeni siku wengine wanachinja.”[2]

Ameipokea Abu Daawuud na wengine kwa cheni ya wapokezi ya wapokezi ilio nzuri.

Kwa hiyo wewe na ndugu zako ndani ya ule wakati mpo Pakistan basi mnatakiwa kufunga pamoja nao pale wanapofunga na mfungue pamoja nao pale wanapofungua. Kwa sababu nanyi mnaingia ndani ya uzungumzishwaji huu. Isitoshe kuonekana kwa mwezi kunatofautiana kutegemea na mwandamo. Kikosi cha wanazuoni – akiwemo Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) – wameonelea kuwa kila nchi na mwezi mwandamo wake.

2 – Kutofautiana kwenu na waislamu walioko kwenu inapokuja katika kufunga na kufungua mnaleta tashwishi na ulinganio katika kuulizana maswali mengi, makemeo na kuzusha migogoro na mizozo. Shari´ah ya Uislamu iliokamilika imekuja kuhimiza maungano, maelewano na kusaidiana katika wema na kumcha Allaah na kuacha ugomvi na mambo ya kutofautiana. Amesema (Ta´ala):

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.”[3]

Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipomtuma Mu´aadh na Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwenda Yemen:

“Toeni bishara njema na wala msiwakimbize watu na baadhi wawatii wengine na wala msitofautiane.”[4]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/103-104).

[2] at-Tirmidhiy (697).

[3] 03:103

[4] al-Bukhaariy (3038) na Muslim (1733).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 18/05/2022