16. Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya kilemba na kuna muda uliopangwa?

Swali 16: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya kilemba na kuna muda uliopangwa?

Jibu: Kupangusa juu ya kilemba ni Sunnah yenye kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliopokelewa na Hadiyth ya al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh). Kwa hivyo inafaa kupangusa juu yake. Mtu anatakiwa kupangusa juu ya kilemba chote, au angalau kwa uchache, sehemu yake kubwa. Pia ni jambo lililopendekezwa kupangusa ile sehemu ya kichwa ambayo iko wazi kama vile sehemu ya mbele ya kichwa, kando ya kichwa na masikio. Hakukuwekwa muda wa kupangusa kwa sababu ni kitu ambacho hakikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliweka muda maalum. Jengine ni kwamba usafi wa kiungo chake ni mwepesi kuliko usafi wa mguu. Kwa ajili hiyo haiwezekani kulinganisha. Pale unapokuwa na kilemba basi pangusa na ukiwa hukuvaa kilemba basi futa kichwa. Upangusaji huu haukuwekwa muda maalum.

Lakini kama unataka kusimama upande ulio salama zaidi usipanguse isipokuwa pale unapokuwa na twahara na ndani ya ule muda uliowekwa juu ya soksi za ngozi, hivo ndio vyema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/170)
  • Imechapishwa: 06/05/2021