17. Je, inafaa kupangusa juu ya Shimaagh, chepeo na kofia?

Swali 17: Shimaagh[1], chepeo na kofia zinazofunika kichwa na masikio zina hukumu moja kama kilemba?

Jibu: Shimaagh na chepeo hazina hukumu moja kama kilemba kabisa.

Kuhusu kofia zinazovaliwa wakati wa majira ya baridi zenye kufunika kichwa na masikio na zinaweza vilevile kufungwa kwa kuzungushwa shingoni, hizi ni kama kilemba kutokana na ugumu wa kuzivua. Kwa hivyo inafaa kupangusa juu yake.

[1] Tazama https://ar.wikipedia.org/wiki/كوفية

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/170)
  • Imechapishwa: 06/05/2021