Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ وَطُورِ سِينِينَ وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ

“Naapa kwa tini na zaituni na kwa mlima wa sinai na kwa mji huu wa amani!”[1]

Sinai ni mlima ambao Allaah alizungumza na Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mji wenye amani ni Makkah. Kuhusu tini na zaituni kuna maoni mbalimbali juu yake.

107- Ka´b-ul-Ahbaar amesema:

“Tini ni msikiti wa Dameski na zaituni ni msikiti wa Yerusalemu.”

108- al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Ni mlima na misikiti Dameski.”

109- Khaalid bin Ma´daan amesema:

“Ni Dameski.”

110- Qataadah amesema:

“Tini ni mlima ambao Dameski iko juu yake na zaituni ni mlima ambao Yerusalemu iko juu yake.”

111- al-Hakam amesema:

“Tini ni Dameski na zaituni ni Palestina.”

112- al-Haarith bin Muhammad amesema:

“Tini ni msikiti wa Dameski na zaituni ni msikiti wa Yerusalemu.”

Kuna kundi la wanachuoni wengine waliosema kuwa tini na zaituni katika Aayah ni yale matunda yanayoliwa. Yamepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas, Mujaahid, ´Ikrimah, al-Kalbiy na wengineo.

Lakini hata hivyo vinaweza kufahamisha sehemu zake ardhini kwa kuzingatia ya kwamba vimetajwa sambamba na sehemu mbili ambazo ni takatifu, ambazo ni mlima wa Sinai na mji wenye amani. Sehemu mbili ndio takatifu zaidi ardhini. Hapo ndiko kulidhihiri utume mtukufu na Shari´ah yenye kufuatwa. Karibu Mitume wote walikuwa ni wenye kutokea Shaam ambapo ndio nchi ya tini na zaituni. Huko pia ndiko kulidhihiri utume wa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kutokea mlima wa Sinai ndiko Allaah alizungumza na Muusa. Katika mji wenye amani ndiko alipoanza kufunuliwa Wahy Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Unabii tatu huu ndio unabii na Shari´ah kutukufu zaidi. Mfano wa hayo yametajwa katika Tawraat.

Seiri ni Yerusalemu na vilivyoko pembezoni mwame na Qaran ni Makkah.

Wale wanachuoni waliosema kuwa tini na zaituni vilivyotajwa katika Aayah ni yale matunda yanayoliwa wamepatia kwa kuzingatia kule kuwepo tini na zaituni juu ya ardhi. Mara nyingi tini na zaituni zinaota Shaam.

Wanachuoni waliosema kuwa tini ni Dameski na zaituni ni Yerusalemu na Palestiana wamepatia kwa kuzingatia ya kwamba Dameski na maeoneo yaliyoko pembezoni mwake ndiko mara nyingi kwenye miti ya tini na Palestina na Yerusalemu ndiko mara nyingi kwenye miti ya zaituni.

Wanachuoni waliosema kuwa kunakusudiwa mlima wa Dameski na mlima wa Yerusalemu wamefanya hivo kwa sababu zaituni na tini huota kwenye mlima.

Wanachuoni waliosema kuwa kunamaanishwa msikiti wa Dameski na msikiti wa Yerusalemu wamefanya hivo kutokana na kwamba misikiti hii miwili ndio maeneo takatifu zaidi Shaam na Allaah ndiye anajua zaidi.

[1] 95:01-03

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 123-125
  • Imechapishwa: 10/02/2017