15. Sababu ya kumi na nne ya maisha mazuri: Maisha ni mafupi

14- Mwenye busara anatambua kwamba uhai wake wa kweli ni uhai wa furaha na wenye utulivu na kwamba ni mfupi mno. Hivyo basi, hatakiwi kuufupisha zaidi kwa masikitiko na kuyaacha yakaingia pamoja na kuuchafua. Kwani mambo hayo ni kinyume na uhai sahihi. Atatia ugumu maisha yake sehemu kubwa kwa kule kunyakua misononeko hiyo na mambo mabaya. Katika hayo hakuna tofauti kati ya mwema na muovu. Lakini hata hivyo muumini anayo nafasi kubwa ya kuhakikisha sifa hii kubwa na fungu lenye manufaa duniani na Aakhirah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Wasaa-il-ul-Mufiydah lil-Hayaat-is-Sa´iydah, uk. 29
  • Imechapishwa: 24/06/2020