15. Ni yepi maoni yako kuhusu jambo la kunyanyua sauti wakati wa kulia?

Swali: Ni yepi maoni yako kuhusu jambo la kunyanyua sauti wakati wa kulia?

Jibu: Nimekwishatoa ushauri mara nyingi juu ya wale waliowasialiana nami kutahadhari kutokamana na jambo hili na kwamba inatakikana na kwamba haitakikani. Kwa sababu jambo hili linawakera watu na kuwatia uzito na pia linawashawishi waswaliji na wasomaji Qur-aan. Kinachotakikana kwa muumini ni yeye ajitahidi asisikilizishe sauti yake kwa kilio na atahadhari kutokamana na kujionyesha. Shaytwaan anaweza kumvuta katika jambo la kujionyesha. Anatakikana asimuudhi yeyote kwa sauti na wala asiwashawishi.

Kama inavotambulika baadhi ya watu hawafanyi hivo kwa kutaka kwao. Bali linawazidi pasi na kutaka kwao, jambo ambalo ni lenye kusamehewa ikiwa ni bila kutaka kwao wenyewe. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba:

“ Anaposoma basi kifua chake kinanguruma kama mgurumo wa sufuria kutokana na kulia.”[1]

Vilevile imepokelewa katika kisa cha Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba anaposoma alikuwa hawasikilizishi watu kutokamana na kulia. Pia imepokelewa kutoka kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba kilikuwa kinasikika kilio chake kutoka nyuma ya safu. Lakini haya haina maana kwamba alikuwa anakusudia kunyanyua sauti kwa kulia. Ni kitu kilichokuwa kinamshinda nguvu kutokana na kumwogopa Allaah (´Azza wa Jall). Hapana neno akizidiwa na kilio pasi na kukusudia.

[1] an-Nasaa´iy (1214), Abu Daawuud (904) na Ahmad (04/25).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 14/04/2022