16. Ni ipi hukumu ya imamu kurudiarudia baadhi ya Aayah zinazozungumzia rehema au adhabu?

Swali: Ni ipi hukumu ya imamu kurudiarudia baadhi ya Aayah zinazozungumzia rehema au adhabu?

Jibu: Sitambui ubaya wa kufanya hivo kwa lengo la kuwahimiza watu juu ya kuzingatia, unyenyekevu na kufaidika. Imepokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alirudiarudia maneno Yake (Ta´ala):

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

“Ukiwaadhibu, basi hao ni waja Wako na kuwasaemehe basi hakika Wewe ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima.”[1]

Aliirudiarudia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kumalizia ni kwamba hapana ubaya ikiwa ni kwa lengo zuri na si kwa lengo la kutaka kujionyesha. Lakini ikiwa anahisi kuwa kufanya hivo kunaweza kuwasumbua na kusababisha sauti za kusumbua zitokanazo na kilio na hivyo akaacha kufanya hivo ni bora zaidi ili kusitokee tashwishi. Ama ikiwa kufanya hivo hakupelekei katika jengine isipokuwa unyenyekevu, mazingatio na kuielekea ile swalah basi yote haya ni kheri.

[1] 05:118

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 14/04/2022