15. Mikono inatakiwa kuwekwa juu ya kifua

15- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiweka mkono wake wa kulia juu ya kitanga chake cha mkono wa kushoto, kifundo cha mkono na kigasha[1] na amewaamrisha hilo Maswahabah wake[2].

Wakati mwingine akiushika mkono wake wa kulia kwa wa kushoto[3].

Anaiweka juu ya kifua[4].

Amekataza kuiweka mikono kuiunoni katika swalah[5] na hilo ndilo alilokuwa akikataza[6].

[1] Abuu Daawuud na Ibn Khuzaymah (2/54/1) kwa isnadi Swahiyh. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (485).

[2] Maalik, al-Bukhaariy na Abuu ´Awaanah.

[3] an-Nasaa’iy na ad-Daaraqutwniy kwa isnadi Swahiyh. Katika Hadiyth kuna dalili kwamba ni Sunnah kuushikilia mkono ilihali Hadiyth iliyotangulia inathibitisha kuwa mkono unatakiwa kuwekwa juu ya mwingine. Yote mawili ni Sunnah. Ama yale baadhi ya Hanafiyyah waliokuja nyuma wanayopendekeza kwamba mtu aunge kati ya kushikilia na kuweka, ni Bid´ah. Mfumo wake ni kwamba kidole kidogo na cha gumba cha mkono wa kulia kishikilie kifundo cha mkono wa kushoto na vile vidole vitatu vilivyobaki viwekwe juu yake. Hivyo ndivyo ilivyotajwa katika “ad-Durr” (01/454) ya Ibn ´Aabidiyn. Usihadaike na maneno ya baadhi ya waliokuja nyuma.

[4] Abuu Daawuud, Ibn Khuzaymah (2/54/1) (aliyesema kuwa ni Swahiyh), Ahmad na Abuush-Shaykh katika ”Taariykh Aswbahaan”, uk. 125. at-Tirmidhiy amesema moja katika isnadi yake ni nzuri. Mtu akitafakari atapata kuwa maana yake iko vilevile katika “al-Muwattwa” na katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy. Nimezungumzia kwa undani njia mbalimbali za Hadiyth hii katika “Ahkaam-ul-Janaa-iz”, uk. 118.

Tanbihi

Imethibiti katika Sunnah ya kwamba mikono inatakiwa kuwekwa juu ya kifua. Vinginevyo ima ni dhaifu au havina asli. Miongoni mwa ambao wametendea kazi Sunnah hii ni Imaam Ishaaq bin Raahuyah. al-Marwaziy amesema:

“Ishaaq aliswali Witr pamoja na sisi…. akanyanyua mikono katika Qunuut na akasoma Qunuut kabla ya Rukuu´. Aliweka mikono juu ya kifua au chini ya kifua.” (al-Masaa’il, uk. 222)

Hali kadhalika ndivyo alivyosema al-Qaadhiy ´Iyaadhw al-Maalikiy:

“Mkono wa kulia unatakiwa kuwekwa juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua.” (al-I´laam, uk. 15)

Mfano wa hayo yamepokea ´Abdullaah bin Ahmad aliyesema:

“Nilimwona baba yangu akiweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kitovu pindi alipokuwa amesimama na kuswali.” (al-Masaa’il, uk. 62)

Tazama “Irwaa´-ul-Ghaliyl” (353)

[5] al-Bukhaariy na Muslim. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (374).

[6] Abuu Daawuud, an-Nasaa’iy na wengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 77
  • Imechapishwa: 13/10/2016