14. Mkono wa kulia unatakiwa kuwekwa juu ya wa kushoto

14- Aliweka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto[1].

Alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sisi Mitume tumeamrishwa kuharakisha kukata swawm, kuchelewesha daku na kuweka mikono yetu ya kulia juu ya mikono yetu ya kushoto wakati wa swalah.”[2]

Alimpitia mtu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyekuwa anaswali ambaye alikuwa ameweka mkono wake wa kushoto juu ya mkono wa kulia, akaifungua na kuweka ule mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto.”[3]

[1] Muslim na Abuu Daawuud. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (352)

[2] Ibn Hibbaan na adh-Dhwiyaa’ kwa isnadi Swahiyh.

[3] Ahmad na Abuu Daawuud kwa isnadi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 76
  • Imechapishwa: 13/10/2016