13. Kunyanyua mikono wakati wa Takbiyr

13- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mara akinyanyua mikono pamoja na Takbiyr[1], baada ya Takbiyr[2] na kabla ya Takbiyr[3].

Alikuwa akiinyanyua mikono kwa kuvinyoosha vidole (havitawanyi na wala havibanani)[4].

Alikuwa akiinyanyua usawa na mabega yake[5] na ilikuwa inaweza kutokea akiinyanyua usawa na ncha ya masikio yake[6].

[1] al-Bukhaariy na an-Nasaa’iy.

[2] al-Bukhaariy na an-Nasaa’iy.

[3] al-Bukhaariy na Abuu Daawuud.

[4] Abuu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/62-64), Tammaam na al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

[5] al-Bukhaariy na an-Nasaa’iy.

[6] al-Bukhaariy na Abuu Daawuud.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 76
  • Imechapishwa: 13/10/2016