15. Kukingwa na kupotea na kula maangamivu

Allaah (Ta´ala) amemdhamini ambaye atashikamana na Qur-aan kwamba kamwe hatopotea duniani na wala hatokula maangamivu Aakhirah. Amesema (Ta´ala):

فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى

”Basi atakayefuata uongofu Wangu hatopotea na wala kutaabika.”[1]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Allaah amemkinga yule mwenye kufuata Qur-aan kutopotea duniani wala kula maangamivu.”

Amesema tena:

“Hatopotea duniani na wala hatokula maangamivu huko Aakhirah.”

Kisha akasoma:

فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى

”Basi atakayefuata uongofu Wangu hatopotea na wala kutaabika.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Ambaye atajifunza Kitabu cha Allaah kisha akafuata yaliyomo ndani, basi Allaah atamlinda kutokamana na upotofu duniani na atamlinda pia na siku ya Qiyaamah na Hesabu mbaya.”[2]

[1] 20:123

[2] AmeipoekaRaziynkaamailivyokatika ”Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (1/67).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 21
  • Imechapishwa: 07/05/2023