Wakati ash-Shaatwibiy (Rahimahu Allaah) alipothibitisha msingi juu ya ukamilifu wa dini, akapelekea mambo mawili kutoka kwa yule mwenye kutafakari Shari´ah na akasema:

“Mosi ni kwamba anatakiwa kuitafakari kwa jicho la ukamilifu na si kwa jicho la upungufu. Anapaswa kuizingatia kikamilifu inapokuja katika ´ibaadah na desturi na asitoke nje yake kwa hali yoyote. Kutoka nje ya Shari´ah si jengine isipokuwa ni kutangatanga, upotofu na upofu. Isiweje hivo ilihali kumethibiti utimilifu na ukamilifu wake?

Ipi ni kwamba anatakiwa kuyakinisha kwamba hakuna mgongano wowote kati ya Aayah za Qur-aan wala mapokezi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali zote ni zenye kuafikiana na zenye kupangwa kwa maana moja.”

Mpaka aliposema:

“Wazushi wameghafilika na sharti ya kwanza. Matokeo yake wakataka kuikamilisha Shari´ah.”[1]

[1] al-I´tiswaam (2/822).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 07/05/2023