Uwajibu wa ukweli na ubainifu katika biashara

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي خالد حَكيمِ بنِ حزامٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (البَيِّعَانِ بالخِيَار مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا، فَإنْ صَدَقا وَبيَّنَا بُوركَ لَهُمَا في بيعِهمَا، وإنْ كَذَبَا وَكَتَمَا مُحِقَتْ بركَةُ بَيعِهِما). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

59 – Abu Khaalid Hakiym bin Hizaam (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wenye kuuziana wako katika khiyari muda hawajaachana. Endapo watasema kweli na kubainisha, basi watabarikiwa katika biashara yao. Na endapo watasema uongo na kuficha, basi wataondoshewa baraka katika biashara yao.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Mfano mwingine ni mtu akuuzie kondoo na kusema kuwa kondoo huu ana maziwa mengi na uongo mwingine kuhusu maziwa.  Hili ni kinyume na ukweli. Kwa sababu ameisifu bidhaa kwa sifa zenye kuvutia. Au kwa mfano akauza kondoo aliye na ugonjwa na hakuubainisha na kinyume chake ugonjwa huo akaunyamazia. Huyu hakubainisha.

Tofauti ya ukweli na ubainifu ni kwamba; ubainifu unakuwa katika sifa zenye kuchukiza na ukweli unakuwa katika sifa ambazo zinatakikana. Mtu akisifu [bidhaa yake] kwa sifa isiyokuwa nayo miongoni mwa sifa ambazo zinapaswa, huyu amesema uongo na hakusema ukweli. Akiinyamazia [bidhaa yake] kwa sifa zenye kuchukiza, huyu ameficha na hakubainisha.

Miongoni mwa haya ni yale yanayofanywa na baadhi ya watu wanaweka bidhaa nzuri juu na mbaya wanaiweka chini. Huyu hakubainisha na hakusema ukweli vilevile. Hakubainisha kwa sababu hakubainisha kasoro za tende na hakusema ukweli kwa sababu ameonyesha tende kwa muonekano ulio mzuri na wakati ukweli wa mambo sivyo.

Miongoni mwa haya vilevile ni yale yanayofanywa na wauzaji magari. Wanauza magari yao na huku muuzaji anajua vizuri sana kuwa ina mapungufu. Anamwambia mnunuaji itazame haina kasoro hata moja. Baada ya kuitazama anainunua. Lakini lau angeashiria ina kasoro fulani  asingeliinunua. Wanawapaka watu mchanga wa machoni. Hili ni haramu.

Ama ikiwa mtu hajui kasoro fulani ilio nayo haina neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/322-323)
  • Imechapishwa: 07/05/2023