15. Kifunguzi cha nne cha swawm: Kunusa uvumba, udi n.k.

4 – Kunusa uvumba hali ya kujua na kukusudia kunamfunguza mfungaji. Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi. Kwa sababu uvumba una athari kwenye ubongo. Lakini ukiingia puani mwake au akanusa bila kukusudia, hakumfunguzi mfungaji kwa sababu ya kutokutaka kwake mwenyewe. Amesema (Ta´ala):

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

[1] 02:286

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 36
  • Imechapishwa: 18/04/2023