5 – Mfungaji kutoa damu kwa chuku kunaiharibu swawm na kunamfunguza pia mfungaji kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Abu Daawuud amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kupitia kwa Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[1]

Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mtu al-Baqiy´ siku ya kumi na nane ya Ramadhaan na huku akifanya chuku akaushika mkono wangu na akasema:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”[2]

Kumepokelewa kuhusiana na haya kutoka kwa kundi la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)[3].

[1] Abu Daawuud (2367) na Ibn Maajah (1680).

[2] Abu Daawuud (2367) na Ibn Maajah (1680). Maimamu wengi, akiwemo Ahmad, Ishaaq [bin Raahuwayh], al-Bukhaariy, ´Aliy bin al-Madiyniy na ad-Daarimiy, wameisahihisha.

[3] Tazama ”Tahdhiyb-us-Sunan” (04/511).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 36
  • Imechapishwa: 18/04/2023