17. Kifunguzi cha sita cha swawm: Kutapika makusudi

6 – Kujitapikisha. Kujitapikisha kunamfunguza yule mwenye kufunga kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Hapa ni pale ambapo atajitapikisha kwa makusudi. Lakini akijizuia na matapishi yakamshinda, basi hakumfunguzi mwenye kufunga. Kutokana na yale yaliyopokelewa kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na ambaye atajitapisha basi ni lazima kwake kulipa.”[1]

Ibn Mundhiriy amesema:

“Wanazuoni wameafikiana juu kuharibika swawm ya mwenye kujitapikisha kwa makusudi.”[2]

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

[1] Abu Daawuud (2380), at-Tirmidhiy (720), Ibn Maajah (1676). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan na al-Haakim.

[2] Tazama ”al-Ijmaa´” (49/126) ya Ibn-ul-Mundhiriy.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 37
  • Imechapishwa: 18/04/2023