15. Hadiyth “Akitawadha mmoja wenu kisha akakusudia kutoka kwenda kuswali… “

294 – Ka´b bin ´Ujrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

إذا توضأ أحدكم ثم خرج عامداً إلى الصلاة فلا يُشبكن بين يديه فإنه في صلاةٍ

“Akitawadha mmoja wenu kisha akakusudia kutoka kwenda kuswali, basi asiingize vidole vyake hivi ndani ya vingine. Kwa sababu yuko ndani ya swalah.”[1]

Ameipokea Ahmad na Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi nzuri. Kwa Ahmad imekuja:

دخل على رسول الله صلى الله عليه وسلم في المسجد، وقد شبكت بين أصابع، فقال لى: ياكعب: إذا كنت في المسجد فلا تشبكن بين أصعابك، فأنت في صلاة ما انتظرت الصلاة

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia msikitini kipindi ambapo nilikuwa nimeingiza vidole vyangu hivi ndani ya vingine. Akasema: “Ee Ka´b! Unapokuwa msikitini basi usiingize vidole vyako hivi ndani ya vingine. Uko ndani ya swalah muda wa kuwa unasubiri swalah.”

Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake amepokea mfano wake.

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/237-238)
  • Imechapishwa: 16/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy