14. Hadiyth “Pindi anapotawadha mmoja wenu nyumbani kwake… “

293 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إذا توضأ أحدكم في بيته، ثم أتى المسجد كان في الصلاة حتى يرجع، فلا يقل هكذا، وشبك بين أصابعه

“Pindi anapotawadha mmoja wenu nyumbani kwake kisha akaja msikitini, basi anakuwa ndani ya swalah mpaka atakaporejea. Kwa hiyo asifanye namna hii.” Akaingiza vidole vyake hivi ndani ya vidole vingine.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake na al-Haakim ambaye amesema:

“Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/237)
  • Imechapishwa: 16/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy