46 – an-Nadhwr bin Muhammad al-Marwaziy (a.f.k. 203)
195 – ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq amesimulia kuwa amemsikia an-Nadhwr bin Muhammad akisema:
”Yeyote anayesema:
إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي
”Hakika mimi ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi niabudu na simamisha swalah kwa ajili ya kunitaja!”[1]
ni kiumbe, ni kafiri.”
Kuhusu kumkufurisha anayesema kuwa Qur-aan imeumbwa ni jambo limepokelewa kutoka kwa maimamu wengi wa Salaf katika nyakati tofauti ikiwa ni pamoja na kipindi Maalik na kipindi cha ath-Thawriy, kisha kipindi cha Ibn-ul-Mubaarak na kipindi cha Wakiy´, kisha kipindi cha ash-Shaafi´iy, kisha kipindi cha ´Affaan na kipindi al-Qa´nabiy, kisha kipindi cha Ahmad na kipindi cha ´Aliy bin al-Madiyniy, halafu kisha kipindi cha al-Bukhaariy na kipindi cha Abu Zur´ah ar-Raaziy, kisha kipindi cha Muhammad bin Naswr al-Marwaziy, kipindi cha an-Nasaa’iy, kipindi cha Muhammad bin Jariyr na kipindi cha Ibn Khuzaymah. Wakati huo watu waligawanyika kati ya wale waliothibitisha kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah, wahy Wake na uteremsho Wake na kwamba si kiumbe, na wale waliosema kuwa ni maneno ya Allaah na uteremsho Wake na kwamba n kiumbe. Miongoni mwa dalili zao wametaja pia:
إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
”Hakika Sisi Tumekifanya kisomeke kwa Kiarabu ili mpate kutia akilini.”[2]
Wakasema kitu kilichofanywa (جَعَلْنَاهُ) ni lazima kiwe kiumbe.”[3]
Muda ulivyozidi kusonga mbele al-Ma’muun akashika utawala. Alikuwa ni mtu wa falsafa na akaruhusu vitabu vya kale vifanyiwe tarjama kwenda katika kiarabu. Akawahimiza watu katika ´Aqiydah inayosema kuwa Qur-aan, akawatisha na kuwatia khofu. Watu wengi wakakubali, kwa kupenda na kwa kutokupenda. Miongoni mwa wale waliokataa kumuitikia ni mwanachuoni Abu Mushir wa Dameski, mwanachuoni Nu´aym bin Hammaad wa Misri, mwanachuoni al-Buwaytwiy wa Misri, mwanachuoni wa Hadiyth ´Affaan wa ´Iraaq na Imaam Ahmad bin Hanbal. Matokeo yake akawatia gerezani ambapo akafa na kuzikwa Twarsuus.
Baada yake akashika utawala ndugu yake al-Mu’taswim. Akaendelea kuwapa watu mtihani na akamfanya hakimu wake Ahmad bin Abiy Du-aad kuongoza mtihani huo. Wakateswa na akajadiliana Imaam Ahmad bin Hanbal, lakini akasimama imara. Kulikuwa na changamoto nyingi ambazo ziliwasilisha ugumu mkubwa kwa wanazuoni wa wakati huo. Yule anayetaka kuyatafakari na kujua yaliyofanyika basi asome vitabu vya historia. Vinginevyo akae nyumbani kwake, awasalimishe watu kutokana na shari yake, anyamaze kwa upole au azungumze kwa ujuzi. Kila nafasi ina maneno yake stahiki ya kuzungumzwa na kila vita vina wanaume wake. Hakika miongoni mwa ujuzi ni wewe kusema pale usipojua ya kwamba Allaah na Mtume wake ndio wajuzi zaidi.
[1] 20:14
[2] 43:3
[3] Amesimulia kutoka kwa Ahmad bin Ibraahiym ad-Dawraqiy, ambaye ameeleza kuwa amemsikia al-Hasan bin ´Aliy bin Shaqiyq akiwahadithia. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na wasimulizi wake ni madhubuti.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 173-174
- Imechapishwa: 12/01/2025
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 173-174
Imechapishwa: 12/01/2025
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/144-mtazamo-ambao-maimamu-wote-wameafikiana/