Wa mwanzo kati ya wale waliotajwa waziwazi miongoni mwa Salaf waliotamka wazi kuwa Qur-aan si kiumbe ni ´Amr bin Diynaar, kama ilivyotangulia kutajwa katika wasifu wake (149). Alifariki mwaka wa 126. Sijapata dalili ya wazi na sahihi inayosema moja kwa moja kutoka kwa yeyote miongoni mwa maswahiba zake juu ya suala hilo, isipokuwa maneno ya jumla ya ´Amr bin Diynaar yaliyotangulia katika kitabu hiki. Ninahisi kuwa ilikuwa takiban namna hiyo, kwani kilichothibitishwa kutoka kwao ni kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah pasi na woa kusema kwamba si kiumbe kwa sababu hapakuwa na haja ya kusema hivyo wakati huo. Hili limeashiriwa na Imaam Ahmad bin Hanbal alipoulizwa:
“Je, mtu ana ruhusa kusema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah kisha akakaa kimya?” Akajibu: “Kwa nini akae kimya? Ingemtosha kukaa kimya lau si kwa sababu ya mzozo uliotokea, lakini kwa vile watu waliongea kuhusu jambo hilo, kwa nini basi yeye asiongee pia?”[1]
Kwa sababu hiyo Haafidhw Ibn ´Adiy amesema:
“Haitambuliki kwamba Maswahabah walipekua suala la Qur-aan.”
al-Bayhaqiy ameitoa maelezo na kusema:
”Anachomaanisha ni kuwa haikutokea katika karne ya kwanza wala ya pili kuwepo kwa mtu yeyote aliyedai kuwa Qur-aan imeumbwa, mpaka ikahitajika kukanushwa ´Aqiydah hiyo. Kwa hiyo hakukuthibiti kutoka kwa yeyote kusema kwamba Qur-aan ni kiumbe. Hata hivyo imethibiti kutoka kwao kuiegemeza Qur-aan kwa Allaah na kuitukuza kwamba ni maneno ya Allaah (Ta´ala).”[2]
Ama maneno ya al-Bayhaqiy kutoka kwa Ibn al-Madiyniy kuhusu masimulizi ya Ja’far as-Swaadiyq yaliyotangulia ya kwamba Qur-aan ”si muumba wala kiumbe”:
“Sijui kuwa mada hii ilizungumziwa kabla ya tarehe hii.”[3]
Hii ni kwa mujibu wa maarifa aliyokuwa nayo. Kwani ´Amr bin Diynaar ni wa zamani zaidi kuliko Ja’far. Zaidi ya hayo imepokewa mfano kama hiyo kutoka kwa Zayn-ul-´Aabidiyn ´Aliy bin al-Husayn, ijapo cheni yake ya wapokezi ni dhaifu, ambaye alikufa mwaka wa 93. Huyu aliitangulia kuishi kabla ya wawili hao.
[1] Masaa’il-ul-Imaam Ahmad, uk. 263-264, ya Abu Daawuud.
[2] al-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 244.
[3] al-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 247.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 174-175
- Imechapishwa: 12/01/2025
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Wa mwanzo kati ya wale waliotajwa waziwazi miongoni mwa Salaf waliotamka wazi kuwa Qur-aan si kiumbe ni ´Amr bin Diynaar, kama ilivyotangulia kutajwa katika wasifu wake (149). Alifariki mwaka wa 126. Sijapata dalili ya wazi na sahihi inayosema moja kwa moja kutoka kwa yeyote miongoni mwa maswahiba zake juu ya suala hilo, isipokuwa maneno ya jumla ya ´Amr bin Diynaar yaliyotangulia katika kitabu hiki. Ninahisi kuwa ilikuwa takiban namna hiyo, kwani kilichothibitishwa kutoka kwao ni kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah pasi na woa kusema kwamba si kiumbe kwa sababu hapakuwa na haja ya kusema hivyo wakati huo. Hili limeashiriwa na Imaam Ahmad bin Hanbal alipoulizwa:
“Je, mtu ana ruhusa kusema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah kisha akakaa kimya?” Akajibu: “Kwa nini akae kimya? Ingemtosha kukaa kimya lau si kwa sababu ya mzozo uliotokea, lakini kwa vile watu waliongea kuhusu jambo hilo, kwa nini basi yeye asiongee pia?”[1]
Kwa sababu hiyo Haafidhw Ibn ´Adiy amesema:
“Haitambuliki kwamba Maswahabah walipekua suala la Qur-aan.”
al-Bayhaqiy ameitoa maelezo na kusema:
”Anachomaanisha ni kuwa haikutokea katika karne ya kwanza wala ya pili kuwepo kwa mtu yeyote aliyedai kuwa Qur-aan imeumbwa, mpaka ikahitajika kukanushwa ´Aqiydah hiyo. Kwa hiyo hakukuthibiti kutoka kwa yeyote kusema kwamba Qur-aan ni kiumbe. Hata hivyo imethibiti kutoka kwao kuiegemeza Qur-aan kwa Allaah na kuitukuza kwamba ni maneno ya Allaah (Ta´ala).”[2]
Ama maneno ya al-Bayhaqiy kutoka kwa Ibn al-Madiyniy kuhusu masimulizi ya Ja’far as-Swaadiyq yaliyotangulia ya kwamba Qur-aan ”si muumba wala kiumbe”:
“Sijui kuwa mada hii ilizungumziwa kabla ya tarehe hii.”[3]
Hii ni kwa mujibu wa maarifa aliyokuwa nayo. Kwani ´Amr bin Diynaar ni wa zamani zaidi kuliko Ja’far. Zaidi ya hayo imepokewa mfano kama hiyo kutoka kwa Zayn-ul-´Aabidiyn ´Aliy bin al-Husayn, ijapo cheni yake ya wapokezi ni dhaifu, ambaye alikufa mwaka wa 93. Huyu aliitangulia kuishi kabla ya wawili hao.
[1] Masaa’il-ul-Imaam Ahmad, uk. 263-264, ya Abu Daawuud.
[2] al-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 244.
[3] al-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 247.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 174-175
Imechapishwa: 12/01/2025
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/145-wa-mwanzo-kuzungumzia-mada-hii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)