45 – ´Abdullaah bin Abiy Ja´far ar-Raaziy

193 – Swaalih bin adh-Dhwurays amesimulia:

”´Abdullaah alimpiga ndugu yake kichwani, ambaye alikuwa na ´Aqiydah ya Jahm. Nilimuona akimpiga kwa kiatu chake kichwani mwake na akisema: ”Hapana, mpaka useme:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

Kwa maana ya Yeye kuwa mbali na viumbe Wake.”[2]

[1] 20:05

[2] Mtunzi ameitaja kupitia kwa Muhammad bin Yahyaa adh-Dhuhliy: Swaalih bin adh-Dhwurays amenikhabarisha… Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Ibn Abiy Haatim amemtaja huyu Swaalih na akasema:

“Muhammad bin Ayyuub amesimulia kutoka kwake.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (2/1/406-407))

Hakutaja juu yake ukosoaji wala kumsifu. adh-Dhuhliy pia amepokea kutoka kwake, kama ilivyo katika ilivyotangulia katika masimulizi haya.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 161
  • Imechapishwa: 12/01/2025
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy